Monday, January 30, 2012

UPUNGUFU WA DAMU KIPINDI CHA UJAUZITO(Anaemia in pregnancy)

Upungufu wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.
Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL. 
Kwa kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku anapohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na pindi mimba inapofikisha wiki 28. 

Viwango vya Anaemina.
 Upungufu wa damu unaweza kugawanywa katika viwango vikuu vinne, yaani upungufu wa damu wa kawaida (mild anaemia) ambao ni kati ya 9-11 gm/ml, upungufu wa damu wa kati (moderate anaemia) ambao ni kati ya 7-9 gm/ml, upungufu wa damu mkali (severe anaemia) ambao ni kati ya 4-7 gm/ml na upungufu wa damu mkali zaidi (very severe anaemia) ambao ni chini ya 4gm/ml. 

Mzunguko wa madini ya chuma mwilini.
Kwa kawaida mwili wa mwanamke huifadhi gramu 3.5 mpaka 4.5 za madini ya chuma. Asilimia 75 huifadhiwa kama hemoglobin katika chembe damu nyekundu, asilimia 20 kama ferritin katika mifupa na asilimia 5 inayobaki huifadhiwa katika misuli na vimeng’enyo vingine vya mwili. 
Wanawake wasio wajawazito hupoteza karibu gramu 1 za madini ya chuma kutoka katika seli za mwili zinazokufa kila siku na gramu 1 zaidi kila siku wanayokuwa kwenye hedhi.

Ukubwa wa tatizo.
Upungufu wa damu kipindi cha ujauzito ni tatizo linalowakumba kina mama wajawazito wengi sana, siyo tu Tanzania bali nchi nyingi zinazoendelea. Inakisikiwa kuwa karibu theluthi moja ya wajawazito katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito hukumbwa na tatizo hili.
Kwa mujibu wa WHO, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 56 ya wajawazito huko kusini mashariki ya Asia hukumbwa na tatizo hili. Kwa hapa Tanzania, hakuna takwimu sahihi kuhusu tatizo hili. Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mtoto ikiwemo kifo.

Chanzo cha upungufu wa damu wakati wa ujauzito.
Kipindi cha ujauzito huambatana na mabadiliko mbalimbali ya mwili. Moja ya mabadiliko hayo ni ongezeko la maji (plasma volume) katika mzunguko wa damu. Katika hali hii, pamoja na kwamba kiasi cha damu huonekana kuongezeka, kiwango cha hemoglobini hupungua mpaka kufikia 11.5mg/dl. 
Karibu asilimia 85 ya anaemia wakati wa ujauzito husababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kusababishwa na kula chakula chenye kiasi kidogo cha madini haya au mwili wa mjamzito kushindwa kutunza madini ya chuma ya kutosha kutokana na ama mimba zilizopita au kupoteza kiasi kingi wakati wa hedhi kabla ya kushika mimba. 
Vyanzo vingine ni pamoja na
Upungufu wa folic acid
Ugonjwa wa sickle cell
Lishe duni kabla na wakati wa ujauzito
Kupoteza damu kwa sababu ya kuumia au kuwa na minyoo (hookworms)
Ugonjwa wa malaria wakati wa ujauzito
Ugonjwa wa chembe damu nyekundu ujulikanao kama beta thalassaemia. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaoishi Asia ya kusini, Ulaya ya kusini na Afrika.
Upungufu wa vitamin B12
Ugonjwa sugu wa kuvunjika chembe damu nyekundu (chronic haemolysis) kama vile ugonjwa kurithi wa chembe damu nyekundu (hereditary spherocytosis)
Ugonjwa wa kupoteza hemoglobin kupitia mkojo (paroxysmal nocturnal hemoglobinuria)
Saratani ya damu (leukemia)
Matatizo ya kupoteza damu kwenye njia ya chakula (gastrointestinal bleeding)
Matatizo katika utumbo hasa wakati wa ujauzito.

Vihatarishi vya tatizo.
.Masuala ya kijamii kama vile umri wa mjamzito, kiwango chake cha elimu na uelewa kuhusu afya yake, kama ana mwenza wa kumsaidia kiuchumi, makazi anayoishi vinaweza kuchangia mjamzito kupata upungufu wa damu
.Vihatarishi vingine ni vile vinavyohusu masuala ya uzazi kama vile idadi ya mimba zilizotanguli (waliowahi kuzaa wana hatari ya kupata anaemia kuliko wanaopata mimba kwa mara ya kwanza), kuwa na mimba ya mapacha na kuwa na historia ya kuzaa mtoto njiti
.Vihatarishi vingine vinahusu tabia za mjamzito kama vile uvutaji sigara, unywaji wa pombe na kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito
.Pia kuwa na magonjwa kama vile kisukari, magonjwa ya figo, pamoja na shinikizo sugu la damu

Madhara na upungufu wa damu kwa mama na mtoto.
Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto ikiwemo kifo. Madhara haya ni pamoja na
.Madhara kwa mama kipindi cha ujauzito: kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi kidogo sana, kuhisi uchungu kabla ya muda, kondo la nyuma kutunga pasipostahili, shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka kabla ya wakati.
.Madhara kwa mama wakati wa kujifungua: kupatwa na uchungu usioeleweka na usio wa kawaida, mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani, kupatwa na shock, hatari ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji, na moyo kushindwa kufanya kazi.
.Madhara kwa mama baada ya kujifungua: maambukizi baada ya kujifungua, kizazi kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.
.Madhara kwa mimba na mtoto atakayezaliwa: Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, mtoto kuwa na score ndogo (poor Apgar score), mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress), na upungufu wa damu kwa mtoto
Watoto wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual developmental milestones), uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na hata kifo. Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases)

Dalili.
Mjamzito mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili zozote. Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula, mapigo ya moyo kwenda kasi, na kuchafuka kwa tumbo. 
Wakati wa uchunguzi mjamzito anaweza kuonekana mweupe kuliko kawaida hasa sehemu za viganjani, kucha za vidoleni, ulimi, au macho. Anaweza pia kuwa na dalili za kuvimba miguu.
Dalili nyingine ni kama zilivyoelezwa katika makala iliyopita ya upungufu wa damu.

Vipimo vya uchunguzi.
Uchunguzi wa upungufu wa damu hufanywa kuwa kupima kiasi cha haemoglobin pamoja kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama peripheral smear. 
Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani total iron binding capacity (TIBC), kiasi cha feritin katika damu, kiasi cha folic acid. Katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani bone marrow biopsy kinaweza kufanywa. Hata hivyo hivi si vipimo vinavyofanywa mara kwa mara.

Matibabu.
Mama mjamzito huitaji miligramu 2 mpaka 4.8 za madini ya chuma kila siku. Ili aweze kupata kiasi hiki, inampasa kula kati ya miligramu 20 mpaka 48 za madini ya chuma. Kwa jamii ambayo upatikanaji wa vyakula vyenye madini hayo ni wa shida, suala hili linaweza kuwa gumu sana kutekelezeka, ndiyo maana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mpango maalum wa kuwapa wajawazito wanaohudhuria kliniki madini ya chuma na folic acid ili kufidia pengo hilo. 
Vidonge vya madini ya chuma ni salama, nafuu na njia makini ya kuongeza na kurekebisha upungufu wa damu mwilini. Kwa wajawazito ambao hawawezi kunywa, kwa sababu yeyote ile, njia ya sindano inaweza pia kutumika. 
Wajawazito wanashauriwa kutumia miligramu 60 za madini ya chuma (ferrous sulphate) na 500mg za folic acid kila siku, ambapo utaratibu huu huendelea kwa miezi mitatu mpaka sita ili kuongeza hifadhi ya madini ya chuma mwilini, hata kama kiwango kinachotakiwa kitakuwa kimefikiwa.

Utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma na baadhi ya chakula.
Vikiliwa wakati mjamzito amekunywa vidonge vya madini ya chuma vinaweza kupunguza unyonyaji wake katika utumbo. Kwa upande mwingine baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kama vile matunda ya jamii ya machungwa huongeza uwezo wa utumbo kunyonya madini ya chuma mwilini. 

Vyakula vya kuongeza damu.
Pamoja na mkakati huo, wajawazito hushauriwa pia kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile nyama, maini, mayai, samaki, mimea jamii ya kunde, maharage makavu, mboga za majani, matembele, na mikate iliyoongezwa madini ya chuma.

Matibabu ya upungufu wa damu mkali kwa wajawazito walio katika wiki za mwisho(baada ya wiki ya 32)
Wagonjwa wa kundi hili hutibiwa hospitali. Wengi wanaweza pia kuwa na dalili za matatizo ya moyo, hivyo wanapaswa kulazwa na kupumzika kitandani, na wakati fulani kuongezewa hewa ya oksijeni. Pamoja na kutibiwa matatizo ya moyo, huongezewa pia damu (packed red cells) kwa vile vidonge vya madini ya chuma havitafaa kurekebisha tatizo hili kwa haraka kabla ya muda wa kujifungua kufika. 

Matibabu ya maradhi mengine.
kwa mazingira yetu, magonjwa kama malaria na minyoo huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa upungufu wa damu kwa wajawazito, hivyo basi magonjwa haya hayana budi kutibiwa kikamilifu ili yasilete madhara kwa mjamzito. Wajawazito wanaoishi maeneo yenye malaria kwa wingi hupewa dawa za SP kwa ajili ya kuwalinda wasipatwe na ugonjwa huu. Pia dawa za minyoo za Albendazole au mebendazole hutolewa kwa wajawazito baada ya miezi mitatu ya mwanzo ili kuua minyoo. Ili kuzuia kujiridia kwa minyoo, wajawazito pia hushauriwa kuvaa viatu/kandambili kila wakati, na kuhakikisha miili na mazingira yao yapo safi. 



Friday, January 27, 2012

MADHARA YA UTOAJI MIMBA


Tumegundua kuwa siku zinavyokwenda wakina mama,dada na wanafunzi wanaongezeka kwa kasi katika utoaji mimba kwa visingizio mbalimbali.



SABABU ZA UTOAJI MIMBA.
Kutokua tayari kulea mimba hiyo kwa kuwa hana uwezo au yuko masomoni.
Kutokua tayari kulea mimba hiyo kwa kuwa aliempa mimba ameikataa.
Kutokua tayari kulea mimba hiyo kwa kuwaogopa wazazi au kuchekwa na jamii n.k.
MADHARA BAADA YA KUTOA MIMBA.
Asilimia kubwa ya kuwa mgumba.
Kama mwanamke hajasafishwa vizuri,anaweza kupata infections kwenye kizazi na hatimaye kizazi kutolewa.
Mwanamke anaweza kupoteza damu nyingi hatimaye Kifo.
Vifaa vinavyotumika katika process ya utoaji mimba,visipokua safi anaweza kupata infections kwenye kizazi.


Wednesday, January 25, 2012

MAAMBUKIZO YA WATOTO

Wazazi tunatakiwa kuwadhibiti watoto wetu hasa waliochini ya umri wa miaka kumi, kutochezea maji machafu ili kuweza kuepuka maradhi ya mripuko hasa kipindupindu,kuhara damu,fangus n.k.




Thursday, January 19, 2012

MICHEZO MBALIMBALI YA WATOTO

Ili watoto wetu wakue vizuri,wawe na upeo mzuri,lazima tuwape nafasi ya kucheza.
Watoto wakijifunza kupeperusha kishada
Watoto wakiruka kamba
Watoto wakishindana kukimbia kwa magunia
Watoto wakishindana kukimbia
Watoto wakicheza mpira wa miguu

Wednesday, January 18, 2012

HAPPY BIRTHDAY IDDY

                              Happy 7th birthday my lovely son Iddy, God bless you!
 From your mumy Ghania and family 

Tuesday, January 17, 2012

UMOJA NI NGUVU

Mamaz wapendanao
Hatuachani ng'oo
Cant miss the next meeting
Mamaz Ghania,apendavyo maendeleo hakuna mfano

MAMAZ WAKISIKILIZA KWA MAKINI NA KURIDHIA MAJADILIANO

Mamaz Beatrice na Farida
Mamaz kufurahishwa na maoni
Mamaz Ghania na Diku wakisikiliza kwa makini
Mwanasheri na Jesry wakifurahia mawazo ya mamaz

Mamaz Jesry akifurahi baada ya ushauri wake kukubalika

MAMAZ WAKIWA KWENYE KIKAO

Mkuu wa nidhamu katikati akitoa maoni yake
Mamaz wakiwa kwenye majadiliano
Mamaz Sarah Machimu(Mhasibu)
Mamaz Joyce Mbago(Mwanasheria)
Mamaz Rehema Mbaga(Mwenyekiti)

HAPPY BIRTHDAY GLADNESS

OOOOH MY GOD!!!!!!,IS 2YRS TODAY BUT IT IS LIKE YESTERDAY SINCE WE RECEIVED A SPECIAL GIFT FROM HEAVEN IN MY FAMILY. YES A GIFT,MY DAUGHTER GLADNESS aka CUTE G IS A SPECIAL GIFT IN MY LIFE.THANX GOD. MY LOVELY DAUGHTER IN THIS U R 2ND BDAY, IF I HAD A WISH WHICH COULD EVER COME TRUE, I WOULD WISH THAT ALL URE DREAMS COME TRUE THOUGH BY THIS TIME I MAY THINK THAT U DONT HAVE ANY DREAMS BUT EVEN LATER. MAY U LIVE LONG LIFE WITH FULL OF HAPPINESS CUTE C. HAVE A WOUNDERFUL BIRTHDAY GLADNESS
MAMAZ SYLIVIA

Saturday, January 14, 2012

PNEUMONIA

Pneumonia is an inflammation of lungs caused by bacteria, virus, fungi and other organisms. Inflammation is mainly due to alveoli (air filled sacs) in lungs responsible for absorbing oxygen. Often it begins after an upper respiratory tract infection.Pneumonia is a common illness which is seen at all age groups.It is leading cause for death in older 65 and in children less than 5 years old.

Types:

• Bacterial Pneumonia - it caused by bacteria either pneumococcus or streptococcus pneumonia.

• Walking pneumonia - it is caused by Mycoplasma Pneumonia.

• Aspiration pneumonia - it is caused due to inhaling foreign material by food, secretions from mouth to lungs.

• Atypical pneumonia - these are milder forms and are usually caused by certain bacteria like Chlamydophila pneumonia, Mycoplasma pneumonia, Legionella pneumophila.

• Klebsiella pneumonia - It is a common hospital acquired pathogen, causing urinary tract infections, nosocomial pneumonia, and intraabdominal infections.

• Viral pneumonia - it is caused by virus and is not very serious.

• Community acquired pneumonia (CAP) - it is an serious infection of lungs that is acquired outside of hospital.

• Bronchial pneumonia - this type of pneumonia spreads to several patches of lungs. It is most prevalent in infants, young children and aged adults.

• Fungal pneumonia - it is caused by Histoplasma capsulatum, Coccidioides immitis, Blastomyces dermatitidis, Paracoccidioides brasiliensis, Candida species, Aspergillus species, Mucor species, Cryptococcus neoformans.

• Pneumocystis Pneumonia - it is caused by Pneumocystis carnii. It is seen people with HIV/AIDS or weakened system.

• Lipoid pneumonia - this type of pneumonia is caused due to use of mineral oil like laxative and as a result of aspiration of liquids.

• Nosocomial pneumonia - this type of pneumonia is acquired during or after hospital for another illness.

Wednesday, January 11, 2012

LISHE BORA KWA WATOTO HUWAPA MAENDELEO MAZURI SHULENI

LISHE bora kwa watoto ni changamoto kwa wazazi wengi. Hii ni kutokana na umuhimu wake kwa afya ya mtoto kiakili na kimwili.

Utafiti unaonyesha kuwa ni muhimu kujumuisha lishe bora katika mpangilio wa mtoto anayesoma hasa katika kipindi cha mitihani ili kumsaidia kufaulu katika mtihani wake.

Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa wazazi wengi huwa mbali na watoto wao pale wanapojiandaa na mitihani. Huwa mbali katika kuwaandaa vyema tangu kiakili hadi katika kuwapatia lishe bora.

Vile vile, utafiti huo unaonyesha kuwa jinsi mwili unavyozidi kuwa na afya bora, ndivyo ubongo unavyozidi kupata nguvu na kijana wako anavyoweza kusoma vyema na kuwa na akili nzuri.

Wazazi wengi huzingatia lishe bora kwa watoto pale wanapokuwa wagonjwa na kusahau kuwa lishe bora ni muhimu wakati wote wa ukuaji wa mtoto.

Lakini, vipo vyakula vinavyofaa kwa watoto hususan wale wanaojiandaa na mitihani. Wataalam na washauri katika masuala ya lishe bora kwa watoto wanakumbusha kuwa wakati huu wa mitihani, watoto wanahitaji chakula kitakachoimarisha afya na utendaji kazi wa ubongo wake na kisichomletea usingizi na kitakachomsaidia kufikiri vizuri.

Mfano vyakula vya wanga vinaupa mwili nguvu inayohitajika kufanya kazi. Hakikisha unavigawanya kwa siku nzima kwa kumpa kidogo kidogo katika kila mlo. Vyakula hivi ni kama wali, chapati viazi na muhogo.

Epuka vyakula vyenye sukari nyingi ambavyo vitampa nguvu kwa muda mfupi tu. Aina hii ya vyakula haishibishi ingawa vinampa mtoto nguvu kwa muda mfupi.

Vyakula vya aina hii pia kwa kuwa havina protini vitamin na madini kwa usawa. Aina hii ya vyakula humuacha mtoto akijihisi mzito na mwisho kusinzia.

Chumvi nyingi nayo ni hatari na inaweza kupandisha shinikizo la damu. Chakula chenye mafuta ni hatari kwani kitasababisha usingizi.

Hakikisha chakula cha mwanao, kina aina moja ya chakula kilichojaa protini. Vyakula hivi ni kama samaki, mayai, nyama isiyokuwa na mafuta, maziwa ya mgando, maharage. Aina hii ya vyakula mbali na protini itampa mtoto vitamin na madini.


Kwa upande wa vinywaji ni muhimu sana mtoto kunywa maji ya kutosha. Pia anywe maji ya matunda halisi (juisi).


Ni muhimu kuhakikisha kuwa mtoto anapata vitamin na madini ili kuimarisha afya ya akili na mwili pale anaposoma. Vyakula vyenye madini ni kama nyama ya ngombe, mbuzi na kondoo pamoja na mboga za majani kama spinachi.

Sio vizuri sana kumpa mtoto vidonge vya ziada vya kujaza madini asiyokuwa nayo. Ni vyema ale vyakula halisi kwani vitampa zaidi ya madini anayohitaji. Kumbuka kumpa matunda ya aina mbalimbali kama machungwa, maembe, embe na karoti.

Pia ni vizuri mtoto ale kwa wakati unaofaa. Usipende kumshindisha mtoto na njaa wala usipende ale ovyo ovyo. Chakula kingi huchukua muda kusagwa na kutumia muda mwingi wa ubongo.

Kifungua kinywa wakati wa asubuhi ni muhimu na lazima kwa mtoto hasa katika kipindi cha mitihani. Ni vyema kifungua kinywa kiwe na protini, madini na mboga pamoja na tunda. Kumbuka kupata virutubisho mapema kutasaidia mwili kuvigawanya kwa siku nzima.

Matunda ni moja ya vyakula bora kwa akili. Sukari ya asili katika matunda, hutoa nguvu safi ya kudumu katika mwili kuliko ile sukari inayotengenezwa viwandani.

Mwisho mpe mwanao nafasi ya kupumzika. Apate hewa safi na apumzishe mwili. Pia wakati wa kula asifanye jambo linguine zaidi ya kula ili afurahie chakula chake.

Wednesday, January 4, 2012

HAPPY BIRTHDAY SIAN

We thank for this day, last year the day like this we received a gift from God. SIAN our little angel you are the best of all the gifts ever received in our lives. Thank you so much for being such a lovely child SIAN. You are the most precious gift that God ever sent to us. We wish you the best in your life, and may lord protect and guide you child in your entire life. HAPPY BIRTHDAY SIAN GODFREY MACHIMU, mom and dad loves you so much.
From Mom(SARAH) and Dad(GODFREY)







Mom(SARAH)




Dad(GODFREY)